Manchester washindi Champions

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Manchester united

Penati ya Steven Gerrard iliwafanya Liverpool kuongoza japo kuwa ushindi huo haukudumu baada ya Wayne Rooney, Juan Mata and Jesse Lingard kuzamisha matumaini ya Liverpool.

Zaidi ya watazamaji 50,000 walijazana katika uwanja huo wa Sun Life Stadium nyumbani kwa NFL Miami Dolphins kushuhudia fainali za michuano hiyo ya ya kimataifa ya Champion.

"Imekuwa jambo la kufurahisha kwa mashabiki wetu kwamba tumeweza kuwafunga Liverpool hapa Marekani” anasema mkuu wa Louis van Gaal.

Kiungo wa Liverpool Gerrard mnamo dakika ya 14 alichokoza nyuki ndani yamzinga pale alipofanikiwa kumhada mlinzi Phil Jones na kisha kufung bao la kwanza.

Hata hivyo Rooney akiwa pia ndiye kaptian wa man united mnamo dakika ya 55 alisawazisha bao hilo baada ambapo Javier Hernandez cross akapachika bao la pili na dakika mbili baadae Mata akapigilia msumari wa moto kwa kupachika bao la tatu.

Rooney aliyeng’ara katika mashindano hayo ametajwa na Van Gaal kuwa ndiye mshambuliaji bora wa England.