Huwezi kusikiliza tena

Sam Nyamweya:''Sing'atuki ng'o!''

Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Kenya Sam Nyamweya amesema yeye pamoja na wanakamati wenzake wa FKF hawatajiuzulu.

Haya nido matakwa ya baadhi ya mashabiki wa kandanda nchini Kenya ambao wameshutumu vikali Nyamweya na kamati yake kwa kile wanasema ni uongozi duni ambao umechangia timu ya taifa Harambee Stars kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa Afrika.

Kenya imeng’olewa na Lesotho.

Nyamweya pia amekanusha madai ya ufisadi kwenye shirikisho lake.

John Nene amezungumza na kinara huyu wa FKF