Pepe Reina kwenda Bayern Munich

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pepe Reina

Klabu ya Bayern Munich wameukubali mpango wa kumsajili mlinda mlango wa Liverpool, Pepe Reina.

Klabu hiyo ya ujerumani kupitia mtandao wao wa Twitter wameandika, "Mlinda mlango Pepe Reina yuko tayari kuhama kutoka Liverpool kuja FC Bayern kisha vipimo vya afya vitafuata.

Mwispainia huyo amepoteza nafasi yake kama mlinda mlango nambo moja wa Liverpool kutoka kwa Meneja Brendan Rodgers baada ya kumsajili Simon Mignolet ambapo msimu uliopita alikuwa Napoli.