Arsenal kutoana jasho na Besikitas

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa Arsenal

Kilabu ya Uingereza Arsenal itachuana na kilabu ya Besikitas ya Uturuki katika mechi za mchujo wa kombe la Mabingwa,huku Celtic ya Scotland ikikabana koo na mabingwa wa Slovenia Maribor baada ya kilabu hiyo kurudishwa katika mechi hizo.

Arsenaly imekuwa ikishiriki katika mechi za mchujo wa kombe hilo katika kipindi cha miaka 16 iliopita.

Kilabu ya Celtic ilipoteza kwa mabao 6 kwa moja dhidi ya Legia Warsaw katika michuano ya kufuzu kwa dimba hilo,lakini mabingwa hao wa Poland wakaondolewa kwa kushirikisha mchezaji ambaye hakufaa kucheza.

Katika Ligi ya bara Yuropa Totenham ya Uingereza itapimana nguvu na AEL Limassol ya Cyprus huku Hull City ikichuana na kilabu ya Lokeren kutoka Ubelgiji.

Kilabu ya Besikitas ilimaliza ya tatu katika jedwali la ligi ya Uturuki na wanafunzwa na aliyekuwa kocha wa kilabu ya West Ham pamoja na mlinzi wa zamani wa Everton Slaven Bilic na kikosi chao kinashirikisha aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba alieihama Chelsea mwezi July.