Arsenal yailaza Manchester City 3-0

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal ndio mabingwa wa mwaka huu wa ngao ya Community.

Arsenal ndio mabingwa wa mwaka huu wa ngao ya Community.

Vijana wa Arsene Wenger waliwanyuka mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Wembley.

Mechi hiyo ambayo hujumuisha mabingwa wa kombe la FA dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

Vijana wa Wenger walidhihirisha niya yao mapema kupitia kwa mkwaju wa Santi Cazorla kunako dakika 21 ya kipindi cha kwanza .

Arsenal iliimarisha nafasi yao ya kukata kiu ya miaka kumi tangu watwae tuzo hilo Aaron Ramsey alipoifungia bao lake la pili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bao la Ramsey

Manchester City ilikosa jibu ya mashambulizi ya Arsenal ila mkwaju wa kichwa wa Stevan Jovetic uliogongwa mwamba.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger aliwajumuisha wachezaji watatu wapya aliowasajili majuzi ,mshambulizi

Alexis Sanchez, kiungo Mathieu Debuchy na beki machachari Calum Chambers.

Wachanganuzi wa maswala ya ndani ya timu hiyo wanabashiri kuwa mwalimu Wenger alikuwa anawajaribu wachezaji hao wapya ilikuwatumia katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya premia siku ya jumamosi dhidi ya Crystal Palace.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bao la Cazorla

Kwa upande wao mabingwa watetezi walikuwa bila ya wachezaji wao 8 mahiri lakini kocha Manuel Pellegrini tayari ameshajionea ushindani utakavyokuwa haswa ligi itakapong'oa nanga juma lijalo.

Pellegrini alikosa huduma za Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Fernandinho, Sergio Aguero, Martin Demichelis, Frank Lampard, Bacary Sagna na Alvaro Negredo.

Man City itafungua kampeini ya kutetea taji lake dhidi ya Newcastle wiki ijayo.