Arsenal ni mwiba

Image caption Wachezaji wa klabu ya Arsenal

Arsenal hapo jana imepeleka wameonyesha kuwa wanaweza kuwa mwiba mkali katika ligi kuu ya England kwa msimu huu baada ya kuibamiza bila timu ngumu ya Manchester City kwa jumla ya mabao 3- kwa nunge katika mechi ya ngao ya Jamii mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Wembly.

Mabingwa hao wa kombe la FA walianza kwa kupeleka kilio kwenye kambi ya Man City kwa goli la kwanza lililofungwa na Santi Cazorla dakika 21 kipindi cha kwanza.

Kama hiyo haitoshi Aaron Ramsey dakika ya 42 aliweka mpira wavuni kuandika goli la pili na kuwafanya Man city wazidi kupata kizungungu na kutojua la kufanya kabla ya Oliver Giroud kumalizia karamu ya Arsenal kwa kushindilia msumari moto kwenye kidonda kwenye dakika ya 60 kipindi cha pili na hivyo kusambaratisha vijana hao wa Manuel Pellegrini kwa jumla ya magoli 3 - 0.