Rwanda nje ya mashindano ya CAF

Image caption CAF yaipiga marufuku Rwanda kutoka mashindano yake

Shirikisho la soka barani Afrika limeipiga marufuku Rwanda kutoshiriki mashindano ya kuwania ubingwa wa mataifa utakaoandaliwa mwakani huko Morocco.

Hatua hiyo inafuatia malalamiko kutoka kwa shirikisho la soka la jamhuri ya Congo kuwa Rwanda ilimshirikisha mchezaji Birori Dady ambaye hati zake za kuzaliwa ni tofauti na zile zilizowakilisha kabla ya mechi ya mchujo wa kombe la mabingwa barani Afrika dhidi ya DRC mwezi uliopita huko Pointe-Noir.

Congo imedhibitishia CAF kuwa Dady, ambaye anaichezea klabu ya AS Vita Club mjini Kinshasa, huwa anahati tofauti kabisa ya kuzaliwa na usafiri chini ya jina tofauti.

Image caption CAF inadai Rwanda ilijua vyema Dady alikuwa na uraiya tofauti

Kufuatia madai hiyo kamati ya uchunguzi ilisikiliza pande zote husika yaani Rwanda, Congo na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na mchezaji mwenyewe tarehe 11 Augosti huko Cairo Misri na ikafikia uamuzi huu wa kuipiga marufuku Rwanda kutoka kwenye mashindano ya mwaka hu.

Katika kujitetea kwake shirikisho la soka la Rwanda lilishikilia kukutu kuwa Dady hakuwa na hati zingine za usafiri lakini uchunguzi ulibaini kuwa shirikisho hilo lilitumia majina yake mengine yaani Etekiama Agiti Tady lilipomuita kujiunga na Amavubi Stars.

Caf ilidhibitisha kuwa Dady alikuwa na tarehe mbili za kuzaliwa na hivyo imempiga marufuku kushiriki mashindano yeyote ya kandanda hadi utata huo utakapotatuliwa kuhusu tarehe yake kamili ya kuzaliwa na uraiya wake.

Image caption CAF yaipiga marufuku Rwanda kutoka mashindano yake

Rwanda, mbayo iliilaza Congo katika mikondo yote miwili imeondolewa mashindanoni na hivyo Congo sasa itachukua pahala pake .

Congo sasa itajiunga na kundi A ambapo imeratibiwa sasa kuchuana dhidi ya Nigeria, Sudan na Afrika Kusini.

Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Rwanda Vincent Nzamwita, ameidhibitishia BBC michezo kuwa amepokea mawasiliano kutoka kwa CAF kuhusiana na marufuku hiyo.

CAF haijaweka wazi iwapo marufuku hiyo ndiyo hatua ya mwisho ama kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo itaichukulia RFA hatua zaidi .

Kamati kuu andalizi ya CAF itakutana tarehe 17 mwezi septembea