Barcelona: Suarez kucheza Jumatatu

Image caption Barcelona : Suarez kucheza Jumatatu

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa mshambulizi wao mpya Luis Suarez ataruhusiwa kucheza jumatatu.

Hiyo ni Licha ya kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini katika mechi ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay.

Kocha Enrique anasema kuwa mshambulizi huyo wa Barcelona Luiz Suarez sasa ataruhusiwa kushiriki mechi ya kirafiki jumatatu ijayo kati ya Barcelona na Club Leon ya kutoka Mexico kufuatia masharti mapya yaliyowekwa na mahakama ya rufaa katika michezo CAS.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Barcelona:Suarez kucheza Jumatatu katika mechi ya Kirafiki

Kocha huyo anasema kuwa mshambulizi huyo wa Uruguay anaruhusiwa kujifua pamoja na timu yake mbali na kushiriki katika mechi za kirafiki.

''Suarez amekuwa akifanya bidii sana na kujifua pekee yake kwa hivyo ninaamini kuwa itakuwa vyema akipata dakika chache angalau mbele ya mashabiki wa nyumbani''

Kufikia leo Suarez, amechapa zoezi mara mbili tu na kikosi cha Barcelona kufuatia marufuku hiyo ya tarehe 24 Juni.

Kufuatia rufaa yake katika mahakama ya rufaa katika michezo haijabainika kikamilifu aliruhusiwa kufanya nini lakini suarez anasubiri kwa hamu na ghamu uamuzi kamili kutoka kwa mahakama hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Suarez amejiunga na Barcelona katika vipindi viwili vya mazoezi

Suarez anaendelea hata hivyo kuhudumia marufuku ya mechi 9 za kimataifa na huenda mechi yake ya kwanza ikawa tarehe 26 oktoba dhidi ya wapinzani wao wakuu Real madrid.

Suarez anatarajiwa kujulishwa rasmi kwa mashabiki wa Barcelona jumatatu ijayo katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp.