Burnley kumenyana na Chelsea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mourinho ana changamoto ,wachezaji kadhaa wana majeraha

Ligi kuu ya England ambayo imeanza jumamosi iliyopita itaendelea jumatatu hii ambapo Burnley watawakaribisha Chelsea kwenye uwanja wa Turf Moor.

Burnley huenda wakawatumia wachezaji wake mahiri akiwemo Lukas Yukiviz ambaye amesajiliwa msimu huu wa majira ya joto akiungana na Danny Ings kuunda safu bora ya ushambuliaji kama ambavyo wamejidhihirisha ubora wao katika michezo ya majaribio kabla ya ligi. Mlinda mlango wao pia sasa yupo salama na timamu kuikabili Chelsea baada ya kukosa michezo kadhaa ya majaribio kutokana na majeraha ya hapa na pale.

Chelsea wao huenda kocha Jose Mourinho akawaanzisha wachezaji wake wapya Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis na bila shaka golikipa Thibaut Courtois.

The Blues wana nafasi ya kujaribu uimara wa goti la mkongwe Didier Drogba, huku wachezaji wengine kadhaa wakielezwa kuwa na hofu ya majeraha.