UEFA: hatutambua mechi za Crimea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa shirikisho la UEFA duniani MIchel Plattini

Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limesema kuwa halitatambua matokeo yoyote ya mechi itakayochezwa na kilabu ya kandanda ya Crimea katika mashindano yatakayoandaliwa na shirikisho la soka nchini Urusi.

Wanachama wengi wa UEFA bado wanalichukulia eneo la Crimea kama la Ukraine licha ya Urusi kulichukua.

Jopo la kukabiliana na maswala ya dharura katika shirikisho la UEFA limesema kuwa ijapokuwa soka inaweza kuwaleta watu pamoja wakati wa majanga ni sharti vilabu vifuate sheria zilizopitishwa na wanachama wote 54.