Balotelli kutua Anfield wakati wowote

Haki miliki ya picha getty
Image caption Balotelli atalipwa kitita cha pauni 120,000 kwa wiki liverpool

Mshambuliaji machachari wa Italia, Mario Balotelli amekamilisha taratibu za usajili wa thamani ya pauni milioni 16 kuelekea Liverpool.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City ameridhia mkataba wa muda mrefu na Liverpool,hata hivyo hiyo jana alianza na maumivu baada ya kushuhudia kipigo kutoka kwa waajiri wake wa zamani Manchester City.

Meneja wa Livepool Brendan Rodgers ana matumaini kuwa hatua ya kumpata Balotelli ina manufaa makubwa na inathibitisha thamani ya juu ya klabu yake

Kwa upande wake Balotelli anasema alifanya makosa kuondoka England mwezi Januari mwaka jana na sasa ana furaha kwa sababu karudi England tena na kusema alitaka kwenda Italia lakini akagundua ni kosa.

Rodgers akizungumzia nidhamu ya mchezaji huyo, amesema watamuimarisha kuwa mchezaji bora aliyepevuka kwa kuwa hawana shaka na kipaji chake.

Baloteli ameichezea kwa mafanikio Manchester City kwa miaka miwili na nusu hata hivyo amekuwa akikemewa mara kadhaa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Pamoja na hayo Liverpool inategemea mazuri kutoka kwake huku Rodgers akitarajiwa kumuweka Balotelli kwenye mstari wakati wote atakapoitumikia Liverpool.