Everton yamsajili Etoo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Everton inataka kumsajili mshambulizi nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka 2

Everton imemsajili mshambulizi nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o kwa mkataba mrefu .

Mshambulizi huyo aliruhusiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu uliopita.

Liverpool pia walionesha niya ya kumsajili lakini mchezaji huyo hakuwahi ushindani kutoka kwa Mario Balotelli.

Kwa mujibu wa wandani huko Goodison ,huenda mshambulizi huyo akashiriki mechi ya kufungua msimu baina ya Everton na Chelsea siku ya Jumamosi.

Everton tayari wamemsajili Romelu Lukaku kutoka Chelsea kwa gharama ya pauni milioni £28m mbali na kumsajili Christian Atsu wa mkopo.

Mshambulizi huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji nyota barani Afrika kwa miaka minne aliifungia Anzhi Makhachkala mabao 12 katika mechi 35 alizoshiriki.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Etoo aliwahi kuhudumu chini ya Mourinho akiwa Inter Milan

Eto'o pia amewahi kuichezea mahasimu wakuu katika ligi kuu ya Uhispania Real Madrid na Barcelona.

Alipokuwa Nou Camp, alitwaa ubingwa wa ligi ya Ulaya mara mbili katika mwaka wa 2006 na 2009 .

Eto'o alijiunga na Inter Milan 2009 kutokea Barcelona alipoisaidia kutwaa kombe la mabingwa chini ya Mourinho huko San Siro.