Manchester City yaibana Liverpool 3-1

Image caption Manchester City yailaza Liverpool 3-0

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza walifungua kampeini ya kutetea taji lake kwa kuinyuka washindi wa pili msimu uliopita Liverpool mabao 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani Etihad.

Stevan Jovetic alipeleka kilio kwa Liverpool kwa kutikisa wavu mara mbili katika kila nusu.

Liverpool ambayo ilijitahidi kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo ilishindwa kutumia vizuri fursa ilizopata haswa katika kipindi cha kwanza ilipobainika itambidi Kocha Brendan Rodgers kutafuta mshambulizi mbadala baada ya kumuuza Luis Suarez.

Hata hivyo Rodgers atakuwa akitafuta ufufuo baada ya kumsajili mshambulizi wa Italia Mario Balotelli kwa pauni milioni 16 .

Uwanjani matumaini ya Liverpool kunusurika kichapo yaliambulia patupu , Sergio Aguero sekunde 23 baada ya kuchukua pahala pake Edin Dzeko.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ushindi huo ni wa pili kwa kwa Man City msimu huu

Liverpool ilipata bao la kufutia machozi baada ya Pablo Zabaleta kujifunga mwenyewe katika dakika 20 za mwisho .

Liverpool itakumbuka Jovetic alipowahangaisha alipokuwa Fiorentina kwa ni jana ndiye aliyekuwa mwiba kwa safu yao ya ulinzi.

Meneja wa Manchester City, Manuela Pellegrini amesema kikosi chake kilionyesha mchezo mzuri ambapo matunda yake ni mabao matatu dhidi ya Liverpool.

Pellegrini anasema ni muhimu kujizolea pointi sita kutoka kwenye michezo miwili ingawa mwanzo ulikua mgumu kwao.

Kwa upande wake Rodgers atajiliwaza na hali ya kuwa wamewasajili wachezaji wapya 9 msimu huu kwa hivyo bado anakisuka kikosi chake kwa niya ya kutetea nafasi yao ya pili ama hata kuiboresha nafasi hiyo ya msimu uliopita.