Etoo astaafu soka ya kimataifa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Etoo astaafu soka ya kimataifa

Mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto'o ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.

Mshambulizi huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi .

Kufuatia kauli hiyo mshambulizi huyo sasa atakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani.

"nataka kuwajuza kuwa nimestaafu mashindano yote ya kimataifa ''aliandika Etoo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Mexico

"Ningependa kuwashukuru sana mashabiki wangu kote barani Afrika na duniani kwa mchango wao ."

Mshambulizi huyo wa zamani wa Barcelona, Inter na Real Madrid alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka wa 1997 Cameroon iliponyeshewa 5-0 na Costa Rica.

Mechi yake ya mwisho ya kimataifa ilikuwa dhidi ya Mexico katika kombe la dunia huko Brazil.