Real Madrid kuvaana na Liverpool

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timu za Uingereza kuchuana na wapinzani kutoka Ujerumani katika kombe la mabingwa barani Ulaya

Arsenal imeratibiwa kuchuana na Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mwaka wa pili mfululizo huku Chelsea ikijipata na upinzani wastani wa Schalke 04 , Sporting Lisbon na Maribor.

The Gunners, ambao walifuzu jana kwa mchuano huo kwa msimu wa 17 mfululizo baada ya kuilaza Besiktas 1-0 imejumuishwa katika kundi D dhidi ya Galatasaray ya Uturuki na Anderlecht.

Kwa Upande wao Mabingwa wa lig kuu ya Uingereza Manchester City watachuna na Bayern Munich , CSKA Moscow iliyoilaza ilipofuzu kwa mkondo wa 16 bora ,kabla ya kuambulia kichapo cha mabao 4-1 mikononi mwa Barcelona.

Liverpool iliandikisha jina lake katika daftari za kumbukumbu ya soka ya bara Ulaya ilipoilaza Real Madrid 1-0 katika fainali ya mwaka wa 1981 mjini Paris.

Lakini baada ya kufungua msimu kwa matokeo wastani Brendan Rodgers sasa anakibarua kigumu dhidi ya mabingwa hao watetezi wa bara Ulaya katika mkondo wa kwanza .

''kwa mtizamo wangu kurejea tena katika kilele cha kandanda katika bara ulaya ni jambo la kujivunia sana .Kujumuishwa pia na Real madrid katika kundi moja ni tukio la kipekee na ambalo litavutia hisia kali ushindani mkali kwa sababu wao ndio mabingwa wa tetezi wa kombe hilo''alisema Rodgers kupitia mtandao wa Liverpool.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Droo ilifanyika Alhamisi Monte Carlo

"tayari ninavutia taswira ya mechi baina ya mabingwa real madrid katika uwanja wetu wa nyumbani wa Anfield nafikiri itakuwa mechi spesheli.''alisema Rodgers.

Lazima tumakinike maanake kundi hilo linatimu zingine nzuri tu ,kwahivyo ushindani bila shaka utakuwa mkubwa sana.

I'm already thinking of Anfield on that night. But there are two other good teams in it along with us. It's a tough group but we'll really look forward to the challenge of getting out of the group."

Kwa upande wake mshambulizi nyota duniani na Real Madrid Cristiano Ronaldo alituzwa kama mchezaji bora barani Ulaya.

Ronaldo aliwapiku wachezaji wa Bayern Munich kipa Manuel Neuer na Mshambulizi Arjen Robben.

Kuhusiana na mechi hiyo dhidi ya Liverpool Ronaldo alisema ''bila shaka pambano hilo ni la kufa kupona .Anfield sio uwanja rahisi kuzoa alama lakini unajua tena sisi ni Real Madrid sisi ndio mabingwa tutajitahidi kwa udi na uvumba kushinda Liverpool''.