Liverpool kumenyana na Madrid Uefa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers

Washindi mara tano wa kombe la klabu bingwa barani ulaya Liverpool watakutana mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid.

Liverpool ikiwa imerejea tena kwenye michuano hiyo baada ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka mitano, pia wako kwenye kundi moja na Basel na Ludogorets ya Bulgaria.

Manchester City itakutana na Bayern Munich kwa mara ya tatu katika misimu minne,halikadhalika CSKA Moscow itamenyana na Roma.

Arsenal itakabiliana na Borussia Dortmund katika msimu wa pili,nayo Chelsea itamenyana na Schalke,pia Lisbon na Maribor.