Bayern yamsajili Xavi Alonso

Image caption Bayern Munich yamsajili Xavi Alonso kwa miaka 2

Kiungo wa Uhispania Xabi Alonso ameafikiana mkataba wa miaka miwili na klabu ya ujerumani Bayern Munich .

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amekubali kuondoka Real Madrid katika misimu mwili ijayo.

Xavi alitokea Liverpool alipojiunga na Real Madrid mwaka wa 2009 na alikuwa ameongeza muda wa miaka 2 katika mkataba mpya aliotia sahihi mwezi Januari Bernabeau .

Hata hivyo haijabainika ni kwanini anaondoka kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu ya Ulaya.

Image caption Bayern yaandika mkataba wa miaka 2 na Xavi

Aidha kiungo huyo alikuwa ametangaza kustaafu soka ya kimataifa jumatano baada ya kuichezea Uhispania katika mechi 114.

Xavi anatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari ijumaa baada ya kupita uchuinguzi wa siha huko bayern hapo jana(alhamisi).

kiungo huyo ambaye ameshinda kombe la dunia na Uhispani huko Afrika Kusini mwaka wa 2010 alitokea Real Sociedad kabla ya kujiunga na Liverpool 2004 alipoisaidia kushinda ubingwa wa bara ulaya mwaka huo.