Man U kumsajili beki Daley Blind

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Daley Blind wa Ajax.

Kilabu ya Manchester United ya Uingereza imekubaliana na kilabu ya Uholanzi Ajax Amsterdam kutoa kitita cha pauni millioni 13.8 kumnunua mlinzi wa timu hiyo Daley Blind.

Blind ambaye ana umri wa miaka 24 alikuwa katika kikosi cha Kombe la dunia cha Uholanzi chini ya mkufunzi Louis Van Gaal.

Anaweza kucheza kama beki wa kushoto pamoja na ngome ya kati ya ulinzi.

Iwapo makubaliano hayo yatatiwa sahihi, huyo atakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na kilabu hiyo.

Kilabu ya Manchester tayari imetumia zaidi ya pauni millioni 130 katika msimu huu pamoja na kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kusajili Angel Di Maria kwa kitita cha pauni 59.7 kutoa Real Madrid.

Old Trafford pia imemnunua beki wa kushoto Luke Shaw,mchezaji wa kungo cha kati Ander Herrera na Marcos Rojo.