Radamel Falcao kwenda Manchester United

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Radamel Falcao

Dirisha la uhamisho wa kimataifa katika siku yake ya mwisho,timu ya Manchester United inakaribia kumtia mkononi tena kwa mkopo mshambuliaji mwenye asili ya Colombia,Radamel Falcao.

Radamel amewasili Man United kwa masuala ya uchunguzi wa kiafya,lakini wakati hayo yakijiri nyota wa man United,mshambuliaji mwenye asili ya Mexico Javier Hernandez naicha mkono timu hiyo na kuelekea Real Madrid kwa mkopo pia.

Suala jingine linaloihusisha timu hiyo ya Madrid ni kuondoka kwa mchezaji wa kimataifa kutoka Italia Alessio Cerci anayeelekeza majeshi yake Atletico akitokea Torino kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kwa muujibu wa shirikisho la soka la kimataifa Fifa,ligi kuu tano tayari zimekwisha tumia zaidi ya dola za kimarekani dola bilioni mbili kwa uhamisho kwa mwaka wa jana pekee. Na dirisha hilo la usajili na uhamisho linafungwa rasmi usiku huu.