Msimu wa usajili wakamilika England

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikosi cha Manchester United

Dirisha la kimataifa la usajili limefungwa jana huku Manchester united wakiibuka kidedea.

Man United imevipiku vilabu vingine vya soka baada ya kumnyakua mshambulia nguli Radamel Falcao kutoka klabu ya Monaco kwa kiasi cha pound milioni 6 huo ukiwa ni mkopo wa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa na klabu ya Monaco hadi anafungasha virago na kuondoka ameifungia Monaco ya Ufaransa jumla ya mabao 11 katika mechi 20.

Nao Arsenal wamemchukua mshambuliaji wa Man United Danny Welbeck kwa mkopo wa pound million 16. Matumaini ni makubwa kwa mshambuliaji huyo anayetua katika uwanja wa Emirates huku mashabiki wake wakionyesha Imani kubwa kwake katika msimu huu.