Southampton yamsajili Sadio Mane

Southampton imemsajili mchezaji wa Senegal Sadio Mane kutoka katika klabu ya Austria ya Red Bull Salzburg kwa kima cha pauni milioni kumi.

Mchezaji huyo mwenye umri wea miaka 22, ambaye ameingiza mabao, 45 katika mechi 87, wakati wa msimu wa ligi ya nchi hiyo, anaweza kucheza kama kiungo cha kati , kwa mujibu wa meneja Ronald Koeman.

Southampton pia wamekamilisha hatua za kumsajili kwa mkopo mlinzi wa Ubelgiji Toby Alderweireld kutoka Atletico Madrid.

Alderweireld alisaidia Atletico kushinda ligi ya uhispania ya La Liga ili kuweza kufika fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu uliopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshindia klabu yake mechi 37.

Koeman amenukuliwia akisema Alderweireld ni mlinzi mzuri na mchezaji mzuri sana.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji, ambaye alishinda mataji matatu katika misimu tisa alipokuwa anachezea Ajax kabla ya kuhamia Madrid msimu uliopita, alisema Koeman alimvutia kakama meneja.