Djokovic; Serena watinga nusu fainali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Novak Djokovic

Novak Djokovic alimshinda Andy Murray katika pambano kali la US Open na kufaulu kuingia nusu fainali.

Mchezaji huyo ambaye ndie nambari moja duniani hivi sasa alishinda kwa seti tatu kwa moja 7-6 (7-1) 6-7 (1-7) 6-2 6-4 dhidi ya Murray katika mchuano wa saa tatu na nusu na kumalizikia saa saba na dakika 17 usiku,.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serena William

Katika nusu fainali Djokovic atachuana na Mjapani Kei Nishikori siku ya Ijumaa.

Kushindwa kwake Murray kuna maanisha kwamba hakuweza kufaulu kucheza nusu fainali ya michuano yoyote tangu afanyiwe upasuaji wa mgongo Septemba 2013.

Katika michuano ya wanawake bingwa mara tano wa US Open Serena Williams amefaulu kuingia nusu fainali ya michuano hiyo kwa kumshinda Mtaliano Flavia Pennettaseti kwa seti mbili 6-3 6-2.

Ekaterina Makarova wa Urussi naye pia alifaulu kuingia nusu fainali ikiwa mara yake ya kwanza kufika hatua hiyo katika michuano mikubwa ya kimataifa. Alimshinda Victoria Azarenka 6-4 6-2.