Marin Cilic bingwa US Open

Haki miliki ya picha PA
Image caption Marin Cilic aibuka bingwa

Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan

Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani.

Cilic amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3 , 6-3.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mchezo wa mwisho unawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic ama Roger Federer.

Cilic anakuwa Mkroatia wa kwanza kutwa ubingwa wa moja kati ya mashindano makubwa manne ya tenis duniani tangu kocha wake Goran Ivanisevic abebe ubingwa wa Wimbledon mwaka 2001.