EURO 2016: England yaifunga Uswisi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption England yaifunga Uswisi, Welbeck ang'ara

England imeanza kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya kwa kuifunga Uswisi.

England imeanza harakati hizo za kucheza fainali hizo zitakazofanyika huko Ufaransa baada ya kuishindilia Uswisi mabao 2-0 usiku wa kuamkia leo.

Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck, aliibuka nyota wa kocha Roy Hodgson kwa kazi nzuri ya kutumbukiza kimiani mabao yote mawili, huku akifunga bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo huo uliopigwa mjini Basel Uswisi.