Manchester United yapata hasara

Image caption Manchester United

Manchester United imeripoti kupata hasara kubwa ya kipato chake cha kila mwaka licha ya kuonesha faida nzuri wakati wa uongozi wa David Moyes kama maneja.

Klabu hiyo ya Uingereza, inasema kuwa kipato chake cha kila mwaka kilishuka kwa asilimia 84, ilihali faida yake iliongezeka kwa zaidi ya asilimia ishirini.

Inasema kuwa inatarajia kipato chake cha mwaka 2015 kushuka, kutokana na kuzidi kuandikisha matokeo mabaya, hasa katika mashindano ya ligi kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Aidha, matokeo hayo pia yanaonesha kuwa Moyes na wafanyakazi wake walipata jumla ya Dola milioni nane kama malipo ya kuachishwa kazi mapema mwaka huu baada ya kuwa ofisini kwa chini ya mwaka mmoja.