Van Gaal: United inalenga taji la EPL

Haki miliki ya picha EPA
Image caption United ilisajili ushindi wake wa kwanza msimu huu

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa anapania kuirejesha kombe la ligi kuu ya Uingereza uwanjani Old Trafford.

Kocha huyo alizungumza punde baada ya Man United kusajili ushindi wake wa kwanza msimu huu .

United iliilaza QPR 4-0 uwanjani Old Trafford jumapili.

''Sasa nataka kurejesha taji la EPL: hapa Old Trafford ikiwa sio msimu huu basi katika mwaka wangu wa pili ama wa tatu.''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Van Gaal: United inalenga taji la EPL

''Isitoshe nataka mashabiki wetu washuhudie mechi z ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya.''

Van Gaal, amewahi kushinda mataji ya ligi katika misimu yake ya kwanza akiwa Barcelona na Bayern Munich,na sasa ameagizwa kumaliza katika nafasi tatu za kwanza na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward.

Baada ya kufunga mara mbili pekee katika mechi nne za kwanza vijana wa Van Gaal, wakiongozwa na Angel Di Maria na Ander Herrera , walisajili mabao yao ya kwanza tangu watue Old trafford .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Van Gaal: Naomba mtathmini ufanisi wangu mwisho wa msimu

Mabao mengine ya United yalitiwa kimiani na Wayne Rooney na Juan Mata .

Van Gaal ameomba uwezo wake utathminiwe kwa jinsi atakavyo maliza msimu huu wala sio atashinda nini.

Manchester United imeratibiwa kuchuana na Leicester jumapili ijayo.