Entente Setif kucheza bila Mashabiki

Image caption CAF yapiga marufuku mashabiki wa klabu ya Algeria Entente Setif

Shirikisho la soka la Afrika CAF limeagiza klabu ya Algeria Entente Setif kucheza mechi yake ya kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazemebe bila mashabiki .

Mechi hiyo imeratibiwa kuchezwa tarehe 20 Septemba Setif.

Caf imefikia uamuzi huo kufuatia matukio kadha yanayokiuka mustakabli wa kandanda yaliyotekelezwa na mashabiki wa ES Setif.

CAF ilitumia ripoti za maafisa wake katika mechi zilizoshirikisha Setif katika hatua za mchujo lakini haikudokeza matukio haswa.