Man City yaanza kwa kichapo Uefa

Image caption Man City ilipata kichapo cha goli moja bila jibu

Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.

Goli la Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90

Wakati Man City wakiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode Bridge walitoka sare ya goli moja kwa moja na Schalke.

AC Roma ya Italia wao waliadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.

Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.

Matokeo mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.