Blatter apinga uchunguzi kuchapishwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa FIFA amepinga kuchapishwa kwa ripoti ya uchunguzi ya wakili Michael Garcia

Rais wa Fifa Sepp Blatter amekataa kata katakutangazwa hadharani kwa ripoti iliyotolewa na wakili kutoka Marekani Michael Garcia baada ya kuchunguza madai ya ufisadi unaodaiwa ulishamiri katika mikutano ya kamati kuu ya FIFA iliyotangaza wenyeji wa makala ya 2018 na 2022 ya kombe la dunia.

Wakili huyo alipendekeza ripoti hiyo itangawe wazi lakini Blatter anapinga ''maswala ya ndani ya FIFA kuwekwa hadharani''.

Rais huyo wa FIFA anasema kuwa shirikisho hilo linasimamiwa na kanuni ambazo haziruhusu uwazi huo.

Kauli ya kuchapisha ama kutochapisha sasa inategemea uamuzi wa mkuu wa kitengo cha kupambana na ufisadi katika FIFA Hans-Joachim Eckert.

Makala ya mwaka wa 2018 yataandaliwa Urusi huku yale mashindano ya 2022 yakikadhibiwa Qatar.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa FIFA amepinga kuchapishwa kwa ripoti ya uchunguzi ya wakili Michael Garcia

Mbali na wakili Garcia, makamu wa rais wa FIFA , Jeffrey Webb, mwanamfalme Ali bin Al-Hussein wa Jordan na Jim Boyce pia wametangaza hamu ya kuweka wazi sehemu ya ripoti hiyo.

Blatter,ametangaza niya ya kuwania muhula wake wa tano akiwa uongozini .

Hata hivyo Blatter mwenye umri wa miaka 78 hajawasilisha rasmi ombi lake la kutaka kuwania urais wa FIFA katika uchaguzi ujao.

Kulingana na kanuni za FIFA ombi lake linastahili kuungwa mkono na mashirikisho 5 kati ya 209 ya kandanda na kuwasilishwa kabla ya Januari tarehe 29 mwakani.