Lampard hajawasiliana na Man City

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mchezaji wa zamani wa kimataifa England,Frank Lampard

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England Frank Lampard amesema hajafanya mazungumzo yeyote na Manchester city kwamba watamuongezea muda.

Lampard alifunga magoli matatu katika michezo mitatu tangu alipojiunga na man city kwa mkopo akitokea New York City.

Mkataba wa Lampard utamalizika mwezi Januari mwakani ,lakini Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini juma hili alisema kuwa Lampard anaweza kuendelea kubaki.