Murray ajitetea kuhusu kauli yake

Haki miliki ya picha epa
Image caption Andy Murray alikosolewa kuunga mkono uhuru wa Scottland

Shirikisho la mchezo wa Tennis nchini uingereza limesema kuwa Andy Murray ni mzalendo kwa nchi ya uingereza baada ya kukosolewa kwa kuunga mkono uhuru wa Scottland.

Murray alikosolewa kwenye mtandao baada ya kuandika kwenye mtandao wa tweeter kuwa anaungana na wale wanaosema Ndio..kwa maana ya wanaounga mkono Scottland kupata uhuru wake.

Mkurugenzi mtendaji wa shirikisho hilo Michael Downey amesema anaunga mkono Murray kwa kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia na kuwa ana haki ya kutoa maoni kwa ajili ya mustakabali wa nchi yake.

Murray mwenyewe alisema kuwa hajutii kutoa maoni yake.