Van Gaal asema wachezaji wake wanajaribu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maneja wa kilabu ya Manchester United Van Gaal katikati.

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amekiri kwamba wachezaji wa timu hiyo wanajitahidi kuelewa mbinu zake.

Mkufunzi huyo wa Uholanzi anasimia kilabu hiyo ikiwa na matokea mabaya zaidi tangu msimu wa ligi ya Uingereza uanze,huku ikiwa imejipatia pointi tano pekee kwa mechi tano ilizocheza.

Wikendi hii timu hiyo inatarajwa kupambana na timu ya West Ham.''tunawapatia wachezaji mafunzo mengi '',Van Gaal alinukuliwa akisema.

''Itafikia wakati katika msimu huu ambapo mafunzo tunayotoa yatakuwa si mengi''.

Wakati huu pengine mafunzo hayo mengi mno.

Tangu achukue usimamizi wa timu hiyo mnamo mwezi July tarehe 16,Van Gaal ametumia mbinu tofauti katika timu hiyo mbali na mabadiliko kadhaa katika mtindo wake wa ukufunzi ili kujaribu kuweka filosofia yake.

Kocha huyo aliyewahi kuifunza Ajax,Barcelona na Bayern Munich ana imani kwamba kilabu hiyo itafaidika lakini amekiri kwamba huenda aliwasukuma sana na kwa haraka wachezaji hao kujifunza mbinu mpya.