Keshi kuendelea kuifunza Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Stephen Keshi

Stephen Keshi amesema kuwa ataendelea kukisimamia kikosi cha soka nchini Nigeria katika mechi ya kuwania taji la ubingwa barani Afrika dhidi ya Sudan licha ya kuwa hajasaini kandarasi mpya.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alipoteza nafasi yake ya kudumu baada ya kukamilika kwa mechi za kombe la dunia,lakini akarudishwa kuifunza timu hiyo ya Super Eagles katika mechi zake mbili za mwisho.

Kufikia sasa hajapata tamko lolote kutoka kwa bodi ya shirikisho la soka nchini Nigeria NFF ,lakini anasema ataendelea kuhudumu.

''Ninaendelea kufanya kazi kulingana na mkataba niliotia sahihi na waziri wa michezo Tamuno Danagogo'',keshi aliiambia BBC.

''Bado sijapata tamko lolote kutoka kwa bodi ya shirikisho la soka nchini Nigeria NFF kwa kuwa uchaguzi ulifanyika siku ya jumanne ,kwa hivyo si tatizo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption kikosi cha Nigeria

Kwa sasa lengo langu kuu ni mechi muhimu dhidi ya Sudan mwezi huu kwa sababu ni muhimu kwa sisi kushinda mechi zote.

Keshi ambaye aliiongoza Nigeria kushinda taji la tatu la Afrika mwaka uliopita na kufuzu katika robo fainali za kombe la dunia nchini Brazil ,ni sharti aifufue timu hiyo baada ya kuanza vibaya katika michuano ya kufuzu katika kombe la taifa bora barani Afrika.