''Justin Gatlin haniridhishi'':Lord Cole

Image caption Justin Gastlin

Makamu wa rais wa chama cha riadha cha kimataifa Lord Cole amesema anasikitishwa na hatua ya uteuzi wa Justin Gatlin kuwa miongoni mwa wachezaji 10 walio na ubora wa juu wa mwaka.

Utata huo dhidi ya Justin Gatlin unakuja kutokana na kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli uliosababisha apewe adhabu ambayo kwa sasa amemaliza kutumikia adhabu hiyo.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 32 ni mmoja kati ya wanariadha 10 walioteuliwa na shirikisho la mchezo huo la kimataifa IAAF hatua ambayo inapingwa na makamu huyo wa Raisi wa mchezo huo.

Gatlin msimu aliweza kushiriki mashindano ya mbio za mita 100 na 200 akiwa na umri huo mkubwa wa miaka Zaidi ya 30,ambapo makamu huyo wa Rais chama cha riadha anasema kwa uwezo huo anastahili ila yeye hamkubali bado.

Coe anayetarajiwa kuchukua Urais wa kuliongoza shirikisho hilo anasema msimamo wake upo wazi katika kukabiliana na udanganyifu michezoni ikiwemo kusisimua misuli na kwamba yeye binafsi anapata shida kuwa sana na mkimbiaji huo Gatlin aliyelaiza kutumia adhabu kutokana na matumzi za dawa za kuongeza nguvu.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa mashindano ya riadha mwaka 2012 kule London amesema msimamo wake upo wazi katika kupinga udanganyifu michezoni na hawajawahi kuweka siri katika hilo na anaamini kuwa udanganyifu ni lazima ukomeshwe.