Ferguson ametukosea, asema Roy Keane

Haki miliki ya picha PA
Image caption Alex ferguson na Roy Keane

Mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United Roy Keane amesema kuwa aliyekuwa kocha wa kilabu hiyo alikosea kuwashtumu wachezaji wake wa zamani katika wasifu wake na kwamba haogopi kumkaripia iwapo wawili hao watakutana.

Ferguson alizungumzia kuhusu wachezaji wa zamani wa kilabu hiyo Roy Kea na david Beckam katika kitabu hicho kilichochapishwa mwaka uliopita.Keane aliondoka Old trafford mwaka 2005 baada ya kukosana na Fergurson.

''Nahisi ni makosa makubwa kunishtumu mimi na wachezaji wengine'' Keane mwenye umri wa miaka 43 aliambia Footbal Focus.''tulifanya vyema katika kilabu hiyo ,tuliweza kupata mafanikio ,tulishinda mataji na sasa kocha anatushtumu.

''Meneja ambaye amejipatia mamilioni ya pauni kutokana na jasho letu,alikabidhiwa sanamu na maeneo yaliotajwa baada ya jina lake, na anafikiri anaweza kutushtumu bila mmoja wetu kusema lolote kwa kuwa anadhani ana mamlaka yote.

Nilisema haiwezekani,kwa nini tukubali kusikiza upuzi kama huu.katika kitabu chake Fergurson amedai kwamba Roy Keane ambaye alikuwa kiungo muhimu wa mafanikio ya timu katika miaka 12 aliyoichezea aliendelea kuwa na ushawishi mbaya.

Keane amesema kuwa hadhani kuwa anaweza kumsamehe Fergurson kwa matamshi yake na kuongezea kwamba hajali kusema lolote lililo moyoni mwake kwa meneja huyo wa zamani iwapo watakutana tena.