Ebola:Morocco yataka mechi kuahirishwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ebola

Vyombo vya habari nchini Morocco vinasema kuwa serikali ya taifa hilo imeomba kinyang'anyiro cha kuwania kombe la kilabu bingwa barani Afrika cha mwaka ujao kuahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa awa ebola.

Hatua hiyo iliafikiwa kutokana na pendekezo la wizara ya afya ambayo inataka kuyazuia mataifa ambayo yameathiriwa na ugonjwa huo.

Maafisa nchini Morroco watafanya mazungumzo kuhusu ombi hilo na waandalizi wake ambacho ni chama cha kandada barani afrika CAF wiki ijayo.

Mechi za kufuzu zinazoshirikisha nchi mbili ambazo zimeathiriwa na ugonjwa wa ebola ambazo ni Guinea na Liberia tayari zimehamishwa ikiwamo mechi ambayo ilitarajiwa kuchezwa leo .