Sessay Ajina kuingoza Sierra leone

Haki miliki ya picha AFP
Image caption KIkosi cha soka cha Sierra Leone

John Ajina Sesay amechukua uongozi wa kikosi cha soka cha timu ya taifa la Sierra Leone kutoka kwa Atto Mensah ili kulisimamia taifa hilo katika mechi yake dhidi ya Cameron.

Ni hatua ya hivi karibuni iliozua mgogoro wa ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kati ya Mensa na Sessay.

Wizara ya michezo inamuunga mkono Mensah huku shirikisho la soka nchini humo likitaka Sessay kuchukua ukufunzi huo.

Mensah amekuwa na kikosi cha taifa hilo kwa maandalizi ya mechi hiyo mjini Younde.

Hatahivyo anadaiwa kujiondoa na kumwachia Sessay ambaye anaungwa mkono na shirikisho la soka nchini humo.

''Ninajiondoa kwa niaba ya kikosi hiki na wachezaji wake'',Mensah aliiambia BBC.

Sessay mwenye umri wa miaka 52 aliteuliwa kukiongoza kikosi hicho siku tisa zilizopita baada ya kumkataa Mensah kwa madai kwamba huenda hana leseni sahihi ya UEFA.