Museveni agharamia Uganda Cranes

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amegharamia safari ya timu ya soka ya taifa Uganda Cranes kwenda Togo, kucheza mechi ya marudiano siku ya jumatano ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kundi E.

Msemaji wa Shirikisho la soka nchini Uganda Ahamed Hussen amefahamisha BBC kwamba Rais Museveni amewapatia dolla laki moja na efu arobuni kusafirisha timu ya Uganda Cranes kwenda Togo kwa mechi ya Jumatano.

Hicho ni kikosi cha Uganda Cranes kilichovalia jezi nyekundu yaani yenye kuishia 42 na yenye 40 ni Togo.

Katika mechi ya jumasi Uganda Cranes ilinyamazishwa na Togo kwa bao 1 kwqa nunge hivyo Uganda wanahitaji ushindi mechi ya Jumatano kuongeza matumaini ya nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.

Katika kundi hilo E Ghana ndiyo wanaongoza na alama 5 wakifatiwa na Uganda alama 4, Ginea alama 4 na Togo alama 3