Ronaldo mbele kwa ufuasi Facebook

Haki miliki ya picha Getty

Mchezaji mahiri wa soka Cristiano Ronaldo amekuwa akichana uwanja kwa kuingiza mabao 18 katika mechi 14 msimu huu.

Ronaldo ambaye amewahi kushinda taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka mara mbili, yuko kifua mbele na mabao 13 katika mechi sita za ligi ya Italia.

Yeye sio nyota tu uwanjani bali pia kwenye mitandao ya kijamii na Jumanne hii alitajwa kwa mchezaji wa kwanza kufikisha Likes milioni miamoja kwenye Facebook.

Mtu mwingine anayeonekana kuenziwa sana kwenye mitandao ya kijamii ni mwanamuziki Shakira.

Wanamuziki wengine kama vile Eminem ana Likes milioni Rihanna Likes milioni 90 na ndio wanamuizki ambao labda huenda wakafikisha idadi hiyo ya mashabiki, labda wakiwa na bahati sana.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ronaldo hutumia Facebook kuwajulisha wafuasi wake kuhusu masiah yake binafsi na kimchezo

Ronaldo alitengeza video ya kuwashukuru mashabiki wake na kusema ni hatua kubwa sana maishani mwao.

"nimefurahi sana nimefikisha mashabiki milioni 100 kwenye Facebook. Ni jambo zuri sana kuweza kufikia maishani mwangu hasa kwa kuwa inaniunganisha na watu kote duniani,'' alisema Ronaldo.

Mshindani mkubwa wa Ronaldo uwanjani,Lionel Messi anakaribiana sana na idadi ya mashabiki wa Ronaldo kwenye Facebook akiwa na mashabiki milioni 74.

Vilabu vya wachezaji hao pia vinafuatana kwa ushabiki katika Facebook, Barcelona ikiwa na wafuasi milioni 77 huku Real Madrid ikienziwa na wafuasi milioni 75.

Ronaldo hutumia Facebook, kuwaonyesha mashabiki maisha yake kama mchezaji na pia maisha yake binafasi.