Man U na Chelsea hakuna mbabe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption wametoshana nguvu

Nchini England Manchester United walitoka sare ya goli 1 -1 na Vijana kutoka darajani Chelsea katika uwanja wa Old Trafford.

Haikuchukua muda mwingi punde tu baada ya kuanza kwa kipute hicho, mchezaji mkongwe Didier Drogba akawainua mashabiki wa Chelsea baad ya kufunga goli zuri la kichwa.

Goli hili liliweza kudumu hadi dakika za nyongeza za mchezo huo na kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuamini kuwa wangekusanya point zote tatu kutoka kwa Man U.

Dakika ya 93 ya mchezo Mholanzi Robin van Persie akawainua mashabiki wa timu yake pamoja na kocha wake Louis van Gaal baada ya kuisawazishia timu yake kwa shuti kali la guu la kushoto na kufanya matokeo kuwa ni sare ya 1-1 mpaka kipyenga cha mwisho.

Baada ya kupata goli la dakika za lala salama Kocha Louis Van Gaal hajafurahishwa na timu yake ya Manchester United japokuwa vijana hao wa Old Trafford wameweza kuondoka na point moja muhimu katika mchezo dhidi ya Chelsea uliochezwa katika dimba la Old Trafford. '' hatujatumia faida ya kuwa nyumbani na tungeweza kushinda mchezo huu'' alisema Mholanzi huyo.

Goli la kichwa la Didier Drogba liliisaidia Chelsea kushika usukani katika mchezo huo kabla ya Robin van Persie kusawazisha na kuwasaidia vijana