Ballon d'Or:Bale na Ronaldo waorodheshwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ronaldo na Bale

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ndio mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati wachezaji wanaoshindania tuzo la mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or huku mshambulizi matata wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa kuhifadhi taji hilo

Bale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid kunyakua kombe la kilabu bingwa duniani

Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar

Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich .

Hatahivyo hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa kumng’ata mlinzi wa Italy Giorgio Chiellini.