Scotland nje soka la wanawake

Image caption Soka la wanawake

Timu ya soka ya wanawake ya Scotland imefungwa na Uholanzi magoli 2-0.

Ndoto za timu hiyo kushiriki kombe la dunia mwakani ziliisha usiku wa kuamkia leo kwa kubamizwa mabao hayo mawili na Uholanzi katika mchezo wa mzunguko wa pili wa nusu fainali na kufanya jumla ya magoli kuwa 4-1 baada ya awali kufungwa 2-1.

Kwa matokeo hayo sasa Uholanzi itakutana na Italy katika mchezo wa fainali.