Liverpool hoi, Chelsea haishikiki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli

Ligi Kuu ya England iliendelea jumamosi katika viwanja mbalimbali, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu katika msimamo wa ligi hiyo.

Katika mchezo wa mapema Jumamosi, Liverpool walitandikwa na Newcastle goli 1 -0. Katika rekodi za nyuma Liverpool haijawahi kushindwa dhidi ya Newcastle katika mechi nne walizokutana, Liverpool wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi nyingine mbili. Hata hivyo hakujawahi kutokea sare ya bila kufungana kati ya timu hizi katika mapambano 40 ya Premier League. Kwa mara ya kwanza sare ya kutofungana kati ya Liverpool na New Castle ilikuwa mwezi Februari 1974.

Michezo mingine ya Jumamosi ni kati ya Arsenal ikaidhabua Burnleyv3 -0 huku Chelsea ilisasambua QPR 2 -1 , Everton wakatoka suluhu na Swansea 0 - 0 na Hull City wakiwa nyumbani wakanyukwa na Southampton 1- 0.

Leicester wakatandikwa n a West Brom goli 1 - 0 , huku Stoke City wakitoka sare na West Ham ya 2 -2.

Kati ya michezo itakayochezwa Jumapili, mechi inayosubiriwa na mashabiki wengi duniani ni kati ya Manchester City watakapovurugana na ndugu zao Manchester United. Manchester City wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17, huku Manchester United wakiwa nafasi ya nane na pointi 13.

Mchezo mwingine wa jumalpi ni kati ya Aston Villa na Tottenham.

Matokeo ya mechi za Jumamosi

Newcastle 1 - 0 Liverpool;Arsenal 3 - 0 Burnley;Chelsea 2 - 1 QPR;Everton 0 - 0 Swansea;Hull 0 - 1 Southampton;Leicester 0 - 1 West Brom;Stoke 2 - 2 West Ham