Man Utd haijaimarika asema Pellegrini

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Manuel Pelegrini asema timu ya Man United iko sawa na ile ya msimu uliopita

Manuel Pellegrini amedai kwamba timu ya Manchester United haijaimarika na haina tofauti na ile ya msimu uliopita wakati anapojiandaa kukabiliana nayo siku ya jumapili.

Van Gaal ambaye amesisitiza hana wivu na kikosi cha Pelegrini kilichoshinda ligi mwaka uliopita, anaamini kwamba ushindi katika mechi hiyo ya 168 huenda ukaipa motisha timu yake kufanya vyema msimu huu,baada ya kuwekwa katika nafasi ya saba na aliyekuwa kocha wake David Moyes msimu uliopita.

Bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji Robin Van Persie siku ya jumapili limeinua motisha ya Manchester United huku kilabu hiyo ikitarajia kuimarika tena .

Lakini baada ya kuiongoza Mancity kuicharaza bao 4-1 nyumbani na 3-0 bila ugenini dhidi ya Manchester United msimu uliopita,Pellegrini anadai kwamba bado hajaona ishara za kuimarika kwa kilabu hiyo ya Old Trafford.

Alipoulizwa iwapo anadhani Manchester United itakuwa timu imara itakapozuru katika uwanja wa Etihad,siku ya jumapili zaidi ya ilivyokuwa chini Moyes,Pellegrini alijibu kwamba haoni tofauti ya manchester ya msimu uliopita na msimu huu.