Meyiwa kuwania taji la mchezaji bora

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa mlinda lango wa timu ya Afrika kusini Senzo Meyiwa ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kuwania taji la mwanasoka bora barani Afrika.

Aliyekuwa mlinda lango wa kikosi cha timu ya Afrika ya Kusini marehemu Senzo Meyiwa ni mmoja ya walioteuliwa kuwania taji la mwanasoka bora barani afrika.

Shrikisho la soka barani aAfrika CAF limetangaza majina ya wachezaji 20 watakaowania tuzo hilo la mwaka 2014,mbali na kutoa orodha ya majina 25 ya mchezaji bora wa shirikisho hilo barani Afrika.

Mchezaji wa Ivory Coast ambaye pia ni kiungo wa kati wa timu ya manchester City Yaya Toure ambaye ameshinda tuzo hilo kwa miaka mitatu iliopita ameorodheshwa tena.

Meyiwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa risasi mwezi uliopita,alikuwa amechaguliwa kama nahodha wa timu hiyo mapema mwaka huu .