Chelsea yaisambaratisha Liverpool 2 - 1

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet aliingia na mpira wavuni na kuwa goli dhidi ya Chelsea

Kwa mara nyingine Chelsea imeonyesha ni moto wa kuotea mbali baada ya kuifunga Liverpool 2 - 1 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililotiwa wavuni na Emre Can baada ya kupiga shuti na kumgonga beki mmoja wa Chelsea na kujaa wavuni.

Baadae Chelsea wakaja juu na kusawazisha goli kupitia kwa Gary Cahill baada ya mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet kuingia na mpira wavuni wakati alipokuwa ameudaka. Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa kwa shuti kali umbali wa takribani meta 15 ndani kisanduku cha 18.

Mechi hiyo ya Chelsea na Liverpool katika uwanja Anfiled kunarejesha kumbukumbu zisizofurahisha kwa upande wa Liverpool pamoja na hali yao ya baadaye ambayo si nzuri sana.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa jezi yake ilichanika uwanjani

Ni miezi sita tu ambapo kuteleza kwa nahodha wa Liverpool Steven Gerard kuliisaidia Chelsea kupata ushindi muhimu dhidi ya timu hiyo ya Mersyside, mechi ilioathiri matokeo ya liverpool na ari yao ya kuwania taji la ligi hiyo msimu uliopita.

Awali katika msimu uliopita mwishoni mwa mwezi Aprili ,kombe la ligi hiyo lilionekana likitaka kuelekea Liverpool lakini baadae ndoto hiyo ilifutika kabisa.

Diego Coast alieanza katika mechi dhidi ya Liverpool bado anaonekana ni moto wa kuotea mbali hasa kwa bahati yake ya kufunga magoli.

Mchezaji huyo wa Uhispania awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la paja na aliorodheshwa katika kikosi dhidi ya Maribor katikati ya wili lakini hakucheza.