Gor Mahia ndio mabingwa wa ligi kenya

Image caption Timu ya Gor mahia yabeba taji la ligi kuu

kenyaTimu ya Gor Mahia nchini Kenya ndio mabingwa wa Ligi msimu huu baada ya kuishinda kilabu ya Ushuru mabao 3-0.

Wakicheza mechi yao ya mwisho ya msimu huu Gor kwa jina maarufu K'Ogalo walihitaji kuishinda KRA ili kushinda taji hilo katika mechi hiyo iliyochezewa katika Uwanja wa Moi mjini Kisumu.

Licha ya timu zote mbili kuonyesha mchezo mzuri hususan KRA, mkwaju wa Eric Ochieng mwisho wa dakika za lala salama katika kipindi cha kwanza, na bao lililofungwa dakika chache za kipindi cha pili na mashambuliaji Dan Sserenkuma bila kusahau bao la tatu la Simon Mburu yalifanya mambo kuwa 3-0.

Katika uwanja wa Ruaraka jijini Nairobi,Elly Kalekwa na kikosi chake cha Sofa Paka walidhani kwamba wataicharaza Tusker FC huku nayo Gor Ikishindwa na wana Ushuru ili kuweza kubeba kombe hilo.

Lakini mambo yalienda segemnege upande wa batoto ba Mungu kama wanavyojiita Sofapaka ambao walipata sare ya 2-2 dhidi ya Tusker na hivyobasi kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi.