Je Gervinho ndio chaguo lako?

Tangu kuhamia ligi ya Serie A, Gervinho amekua mmoja wa wachezaji wenye kipaji katika soka la Afrika.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa Roma, mchezaji huyu (27) alifunga magoli 12 katika mechi 37 sambamba na mchezaji mwenzie Francesco Totti na Alessio Cerci ambaye sasa anachezea Atletico Madrid.

Roma iliibuka mshindi wa pili katika ligi ya Serie A na kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza kwa miaka minne.

Kama ilivyo kwa wachezaji wakubwa wa Ivory Coast, akiwemo Toure na Solomon Kalou, Gervinho alianza kucheza soka akiwa kijana na klabu ya ASEC mjini Abidjan.

Huko ndiko Gervais Yao Kouassi kwa mara ya kwanza alipofahamika kwa jina la Gervinho baada ya kupewa jina hilo na Kocha kutoka nchini Brazil.

Gervinho alishiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu.