Je utamchagua Pierre-Emerick Aubamayeng?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pierre-Emerick Aubamayeng ndiye mchezaji pekee ambaye hakucheza kwenye kombe la dunia kati ya walioteuliwa

Mchezaji huyu ameteuliwa tena kwa mwaka wa pili kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za BBC ni mchezaji pekee miongoni mwa washindani watano ambaye hakushiriki michuano ya Kombe la dunia nchini Brazil.

Msimu uliopita aliisaidia Borussia Dortmund katika Bundesliga na Kombe la Ujerumani ambapo Bayern Munich ilijinyakulia ushindi na kufanya timu hiyo kufika mpaka robo fainali za ligi ya mabingwa,na kuondolewa na Real Madrid katika hatua hiyo.

Aubamayeng alizaliwa ufaransa lakini alicheza kwenye ardhi ya baba yake, Gabon.anasema kwa sasa anafanya vizuri Dortmund sababu anaielewa vizuri ujerumani.

Anasema msimu uliopita hakuelewa lugha, ulikuwa ulimwengu mpya kwake.

Mshambuliaji huyu kimataifa ameifanya Gabon kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la mataifa Afrika, baada ya kupata ushindi dhidi ya Burkina Faso