Je utapenda Brahimi anyakue tuzo ya BBC?

Yacine Brahimi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yacine Brahimi

kila mwaka, vilabu vikubwa nchini Ufaransa huwania wachezaji kutoka shule ya Clairefontaine inayowapika vijana.

Mwaka 2006,Yacine Brahimi aliibuka kuwa wa kipekee na kujiunga na Paris Saint-Germain.

Lakini wazazi wake walipendelea asaini mkataba na Stade Rennais, kilabu kinachotoa mafunzo kwa vijana wadogo yaani chipukizi.

lakini mipango yake haikwenda vizuri,Brahimi alikua dhaifu kutokana na kuwa majeruhi pia alikua na mikwaruzano ya mara kadhaa na kocha Frederic Antonetti.

Hatua ya kuhamia Granada ilimpatia kiungo huyo wa kati mwanzo mpya nchini uhispania na kuaminiwa sana kuliko ilivyokua nchini ufaransa.

Hata hivyo pamoja na mtindo wake wa uchezaji kushangiliwa sana uhispania , alikuwa akikosolewa kutokana na umaliziaji wake kutokuwa wa kuzaa matunda.

Katika misimu miwili na zaidi ya michezo 60,Brahimi alifunga magoli matatu pekee na kusaidia kupatikana kwa magoli matano .

Nchini Ureno Brahimi aling'ara , baada ya kufunga magoli manne katika mechi 11 na kusaidia kufunga kwa magoli mengine manne.

Hivi sasa Yacine Brahimi anaichezea Porto akivaa jezi namba nane.